Halmashauri ya Mji wa Bunda inapenda kuutangazia Umma na wakazi wa eneo la Halmashauuri ya Mji wa Bunda kuwa inakusudia kutunga sheria Ndogo kwa ajili ya kuhifadhi mazingira. Sheria hii itajulikana kama sheria ndogo za Halmashuri ya Mji wa Bunda (Hifadhi ya Mazingira) za mwaka 2022. Rasimu za sheria ndogo hizi imeambatanishwa pamoja na Tangazo hili kwaajili ya rejea.
Kwa hali hiyo, Taasisi, Kampuni, Mtu binafsi au Kikundi cha watu wanaruhusiwa kuwasilisha maoni au pingamizi kwa njia ya maandishi kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji kupitia Ofisi ya Mtendaji wa Kata kuhusiana na kusudio la utungwaji wa sheria ndogo hizi. Pingamizi au maoni hayo yawasilishwe kabla au kufikia tarehe 30/03/2022.
Bofya hapa kutazama RASIMU HIYO. SHERIA NDOGO ZA HIFADHI YA MAZINGIRA.pdf
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda