Leo tarehe 15.08.2022, Benki ya ABC kupitia Meneja wa Kanda Ndg. Davis M. Kalumuna imekabidhi Kompyuta Moja kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kwaajili ya matumizi ya Ofisi.
Akipokea Kompyuta hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel J. Mkongo kwa niaba ya Watumishi wote wa Halmashauri, ameipongeza na kuishukuru Benki ya ABC kwa ushirikiano mzuri inayoufanya dhidi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Aidha Mkurugenzi amesema kuwa Benki ya ABC imeonesha mfano mzuri wa kuitikia kwa haraka zaidi pale walipopokea na kulifanyia kazi ombi la vitendea kazi vya Kielectroniki vitakavyoweza kusaidia Watumishi wa Halmashauri kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Awali, Bwana Davis M.Kalumuna Meneja wa Benki ya ABC Kanda ya Ziwa, amesema walipokea barua hiyo kutoka kwa Mkurugenzi na kuahidi kuifanyia kazi. Anasema baada ya kupokea ombi hilo benki imeamua kutoa Kompyuta Ili kuunga Mkongo juhudi za Maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ili kazi iendelee.
Hata Hivyo, Meneja wa Benki hiyo ameahidi kuendeleza ushirikiano wa kutosha kwa Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa mikopo rahisi kwa Watumishi, Mikopo ambayo ni ya Chapuchapu kwa riba nafuu.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda