Leo Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Bwn. Dotto Makota amemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney madawati 100 kwaajili ya wanafunzi wa shule ya Msingi Bigutu.
Tukio hilo adhimu limetokea katika shule ya Msingi Bigutu ambapo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda ameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kurudisha shukrani kwa wananchi kwa kutoa Madawati 100 kwaajili ya wanafunzi wa shule ya Msingi Bigutu.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema, NMB ni Taasisi kubwa yenye uwezo wa kutoa Madawati mengi zaidi ya hayo, hivyo amewaomba kuendelea kutoa zaidi kwani Bado shule nyingi zinauhitaji wa Madawati.
Akimwakilisha Meneja wa NMB Kanda Bwn. Dotto Makota amesema walipopokea ombi la kuchangia Maendeleo kutoka shule ya Msingi Bigutu walifarijika sana na kuamua kulifanyia kazi ombi hilo kwa haraka na hatimae Leo hii wameweza kukabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi 12,036,000/-
Kwa upande wake wake Diwani wa Kata ya Bunda stoo Mheshimiwa Flavian Nyamageko ameishukuru sana Benki ya NMB kwa kusikia kilio Chao Cha madawati na kuamua kuwasaidia. Aidha ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa jitihada kubwa inazofanya kuhakikisha Kata yake na Wilaya kwa ujumla inanufaika na misaada mbalimbali ya maendeleo kama ilivyofanikisha jambo hilo la Madawati.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda