Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Leo umefika katika Kata ya Bunda stoo kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo ikiwa ni mwendelezo wa kuzunguka Kata kwa Kata kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Wakazi wa Bunda stoo walipata fursa ya kueleza kero zao zilizolenga sekta mbalimbali za ubovu wa barabara, kufikishiwa huduma ya Maji katika Maeneo ambayo hayajafika, mahitaji ya eneo la kuweka Soko kusogeza huduma karibu, shida ya umeme kukatika mara kwa mara, mifugo kuzurura hovyo kula miti na mazao, mbwa kuzurura na kero nyingine nyingi.
Viongozi walioguswa na kero za wananchi walisimama na kujibu hoja baada ya hoja. Kwa kero ambazo hazikuweza kutatuliwa katika eneo la Mkutano Viongozi waliahidi kuzifanyia kazi na kuleta mrejesho kupitia kwa Afisa Malalamiko wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwana Arende.
Mwisho Wananchi wamefurahi sana kwa kusikilizwa na kutatuliwa kero zao lakini pia wameomba Halmashauri kutafuta aina mpya ya mazao ya Biashara yanayoendana na hali ya hewa ya eneo hili kutokana na tabia Nchi kubadilika mara kwa mara.
#kaziiendeleee
See translation
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda