Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Dkt. Vicent Anney amewataka na kuwaagiza wazazi kuchangia chakula shuleni kwaajili ya watoto kula wawapo shuleni ili wapate muda wa ziada na nguvu ya kutosha kujifunza.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda amesema hakuna shule ya mfano katika kutoa Elimu Bora katika Halmashauri ya Mji wa Bunda huku akiitaja shule ya Sekondari Bunda pekee kuanza kujitahidi kuinua Taaluma na kusema anataka shule mpya ya Sekondari ya kata ya Bunda Mjini iwe mfano wa kuwa na matokeo mazuri na ikiwezekana ifanane na shule ya Kata ya Kismili Mkoani Manyara ambayo wanafunzi wake wanapata Daraja la kwanza na wakifeli basi wanapata daraja la pili.
Dkt. Anney amesema matokeo mazuri hayawezi kuja kama wazazi hawaoneshi ushirikiano wa kuwapatia watoto wao chakula shuleni. Ameongeza kusema kuwa Serikali kwa upande wake inatekeleza wajibu wake wa kuboresha Miundombinu ya Elimu nchini na kwamba imebaki nafasi ya Wazazi kuonesha mchango wao kwa kuwapatia wanafunzi chakula shuleni.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda