Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney akilihutubia Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda amelishauri Baraza kuzingatia vipaumbele muhimu katika Mapango na Bajeti wa Mwaka 2025/2026.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema anapenda kuona Halmashauri inaongeza Mapato ya Halmashauri kwa kusimamia vizuri vyanzo vya Mapato na kudhibiti mianya ya wizi. Na pia Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameelekeza kubuni na kuongeza Vyanzo vipya vya Mapato ikiwa ni kufaidika na Kampuni zinazochimba Madini ndani Halmashauri kupitia Corporate Social Responsibility CSR.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema pia Bajeti hiyo izingatie kulipa madeni ya Wafanyabiashara na kulipa fidia za Ardhi kwa wananchi ambao Maeneo yao yametwaliwa kwa shughuliza za Serikali.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuhusu usimamizi wa miradi na kumaliza kwa wakati ili kuepusha miradi viporo.
Mwisho Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesisitiza pia ufuatiliaji wa wanafunzi ambao hawajaripori shule tangu shule kufunguliwa kutafutwa na kuhakikisha wanaripoti katika shule zao.
#kaziiendeleee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda