Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Juma Chikoka, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma amewataka watendaji wa kata kuweka mkazo na msisitizo kwa wazazi na walezi kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni. Mheshimiwa Chikoka amesema huwezi kutenganisha elimu na chakula kwa watoto.
Hayo yamesemwa katika kikao cha tathimini ya lishe robo ya nne katika wilaya ya Bunda kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo kimehusisha Halmashauri zote mbili Bunda Mji na Bunda DC.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amezitaka Halmashauri kuweka ushindani na kutoa motisha kwa kata ambazo zitafanya vizuri na kuongeza nguvu kwa kata ambazo zinahitaji nguvu zaidi. Mbali na hilo, Mheshimiwa Chikoka amewataka viongozi wa kata kubaini changamoto au watu/makundi ya watu wanaokwamisha kampeni ya lishe kutekelezwa kwa ufanisi na kuwachukulia hatua.
Mwisho, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha utekelezaji wa kampeni ya lishe unafanikiwa kwa asilimia mia ili kuleta matokeo chanya kwa watoto na jamii kwa ujumla.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda