Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney leo amekutana na makundi mbalimbali ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji Bunda ambao ni watumishi wa Makao makuu ya Halmashauri, Watendaji na Watumishi wa Idara ya Afya kusikiliza mahitaji yao, kero na maoni mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu ya Kila siku.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alitoa fursa kwa watumishi kueleza hisia zao, kero na kutoa maoni katika Mazingira wanayofanyia kazi ambapo watumishi waliitumia ipasavyo kuelezea yanayowakabili katika utendaji wao.
Ikiwemo madai ya mishahara, stahiki mbalimbali za kiutumishi n.k
Baada ya kusikiliza maoni ya Watumishi, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alitoa maagizo kwa Uongozi wa Halmashauri kuzingatia stahiki mbalimbali zinazowahusu watumishi wenye madai ikiwemo kuwabadilishia miundo watumishi wenye sifa na kuwapa fursa mbalimbali zitakazowasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameelekeza pia watumishi kutunza Siri za Ofisi, kulinda na Kuhifadhia Mali za Umma ikiwa ni pamoja na kufanya mawasiliano baina yao ili kuboresha utendaji.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewaonya wafanyakazi kuepuka Mikopo chechefu inayodharirisha Utumishi wa Umma na kuridhika na mishahara yao ikiwa ni pamoja na kubuni miradi mbalimbali itakayowasaidia kujiongezea kipato Chao.
Mwisho amewataka watumishi kudhibiti na kutoa taarifa za kiuhalifu katika Maeneo yao ili kulinda amani na Usalama hasa kwa Watendaji wa Kata na Mitaa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda