Tarehe 07.09.2022
Mheshimiwa Joshua Nassari Mkuu wa Wilaya Leo katika Baraza ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani kuepuka Migongano na marumbano yasiyokuwa na tija dhidi ya wao kwa wao na Watumishi wa Halmashauri. Amesema Halmashauri ya Mji wa Bunda inafanya kazi vizuri kutokana na ushirikiano uliopo baina yao na Watendaji Hivyo amewaasa kuendeleza ushirikiano huu uliopo na kuzidisha Mshikamano.
Katika sura nyingine, Mheshimiwa Joshua Nassari ametoa taarifa ya mbolea ya ruzuku itakayouzwa kwa bei nafuu hivyo kuwataka Waheshimiwa Madiwani Kuhamasisha Wakulima waliopo katika maeno yao kujisajili katika Ofisi za Watendaji wa Mitaa na Maafisa Kilimo waliopo katika Mitaa yao. Mheshimiwa Nassari amesema utaratibu huu umeboreshwa na upo kitaalamu zaidi Ili kuimarisha usimamizi na udhibiti wa udanganyifu kwa Wakulima na Wataalamu kwa ujumla.
Aidha, Mheshimiwa Nassari ametoa taarifa ya mahindi ya gharama nafuu kwamba yataletwa Wilayani Bunda muda si mrefu Ili kupunguza ukali wa gharama za Chakula. Pindi mahindi hayo yatakapotolewa taarifa itatolewa kwa Umma.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya hakusita kuwakumbusha Waheshimiwa Madiwani kuwa Miradi yote inayotekelezwa katika Kata zao ni Miradi ya Halmashauri Hivyo kila mmoja anawajibu wa kuiunga mkono na kuisimamia kwa Maendeleo ya Halmashauri nzima.
Mwisho Mheshimiwa Nassari amewataka Waheshimiwa Madiwani kutowakatisha tamaa ya kufanya kazi Watendaji wa Serikali Ili waweze kufanya kazi kwa moyo na kila mmoja azingatie mipaka ya kazi yake.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda