Leo Kamati ya Mipangomiji na Mazingira ya Halmashauri ya Mji wa Bunda imefanya ziara ya kupitia Maeneo mawili ya wananchi wanaoomba kibali Cha kubadili matumizi kama ifauatavyo; Kiwanja namba 165 block "N" kutoka kuwa kiwanja cha Makazi kuwa kiwanja Cha Biashara na Kiwanja namba 1786 block "N" kutoka makazi kuwa kiwanja Cha Kituo Cha Afya.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Mhe. Mzamil Kiwanila imeyaona Maeneo hayo yote mawili na kuahidi kuyafanyia kazi katika Vikao ambavyo vitapangwa na Halmashauri ili kujiridhisha na hatua mbalimbali kabla ya kuridhia maombi hayo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda