Miradi hii ni utekelezaji wa kipindi cha Januari - Juni 2024 na Julai - Desemba 2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda Mhe. Mayaya Ibrahimu Magese na timu yake wamepongeza usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo unaofanywa na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Aidha Kamati imetoa maelekezo kwa mapungufu yaliyobainika kufanyiwa kazi na maeneo yenye uhitaji serikali ihakikishe inafanyia kazi ili miradi ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma.
Kwa upande wa Serikali Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda ameieleza Kamati kwamba wamepokea maoni yote na maelekezo na ameahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
Miradi iliyotembelewa ni shule mpya ya Sekondari ya Nyasura, Ujenzi wa Mabweni mawili shule ya sekondari Kabasa, ujenzi wa Madarasa shule ya msingi Mbugani, zahanati ya Kitaramaka Sazira na ujenzi wa barabara ya Korongoni Nyasura.
Kamati ya Siasa ilitembelea pia, kata ya Nyatwali na kuongea na wakazi ambao bado hawajalipwa fidia. Mheshimiwa Mwenyekiti amewaondoa wasiwasi wakazi hao ya kwamba wawe na subira wakati serikali ikiendelea kukamilisha taratibu za malipo yao.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda