Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndg. Gerald Kusaya ameongoza kikao Cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga ukatili dhidi ya Wazee itakayofanyika Kitaifa tarehe 15.06.2024 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Miembeni Wilayani Bunda.
Katibu Tawala amesema katika kuadhimisha siku hii, Kutakua na mfululizo wa siku Tatu za matukio mbalimbali kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi wa sita ambayo ndio kilele Cha maadhimisho hayo.
Matukio yatakayokuwepo ni Kongamano litakalofanyika katika Chuo Cha Ualimu Bunda, Kutembelea Kaburi la Baba wa Taifa Butiama, Michezo mbalimbali ya Wazee, Upimaji wa Afya itakayofanyika viwanja vya shule ya Msingi Miembeni na mwisho siku ya kilele kutakua na Burudani mbalimbali pamoja na salamu kutoka kwa Viongozi wa Kitaifa na Mkoa.
Aidha Katibu Tawala amesema kuwa Mgeni Rasmi wa siku ya kilele Cha maadhimisho haya anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Mwisho Katibu Tawala amewaalika wananchi wote ndani na nje ya Mkoa wa Mara kuja kushiriki maadhimisho haya.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda