Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Bunda chini ya Mwenyekiti Ndg. Salum Mtelela Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda kwa niaba ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya imekaa leo kusikiliza na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Taasisi za Serikali zilizopo katika Wilaya ya Bunda na kisha kushauri baadhi ya maeneo ili kuhakikisha mambo yote yanaenda kama yalivyopangwa.
Taasisi zilizowasilisha taarifa ni Halmashauri ya Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, TRA, TANESCO, NIDA, Chuo Cha Ualimu Bunda, Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Kisangwa, BUWSSA, RUWASA, Bodi ya Pamba, TARURA, TFS, na TSC.
Aidha, katika kuhakikisha mambo na mipango inaenda kama ilivyopangwa, Mheshimiwa Mwenyekiti amesisitiza Umoja na mshikamano hata kwa walionje ya Taasisi husika kufanya kazi kwa pamoja na kwa kutegemeana ili kuunganisha nguvu.
Mwenyekiti amegusia pia suala la Elimu kwamba bado Elimu ya Bunda kwa wanafunzi hairidhishi hivyo amewataka wajumbe wote kwa pamoja kuungana kuhakikisha kiwango Cha Elimu kinapanda katika viwango vinavyotakiwa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda