Leo tarehe 15.11.2022 Halmashauri ya Mji wa Bunda imeendesha mafunzo elekezi kwa watumishi Ajira Mpya takribani 39 toka Idara ya Utumishi na Utawala, Afya, Fedha, Kilimo na mifugo pamoja na Kitengo Cha Ujenzi.
Wakati akiahirisha mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bw. Emmanuel J. Mkongo amewaasa Watumishi hao kuwa waadilifu kuepuka Tabia sizizofaa kama unywaji wa pombe muda wa kazi, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hasa kuepuka kushiriki mijadala isiyofaa ya kuichafua Serikali mitandaoni.
Aidha amezidi kusisitiza ushirikiano kazini utunzaji wa siri za Ofisi, kushirikisha Ofisi pale wanapokutana na changamoto mbalimbali za kiutendaji na zaidi kuyashika yale yote waliofundishwa na Wawezeshaji wa Mafunzo.
Upande mwingine Wawezeshaji wamewaasa Watumishi hao kuzingatia Sheria na taratibu zote za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao kazini na pia kuepuka vishawishi vinavyopelekea uvunjifu wa Sheria hasa kuridhika na kipato wanachokipata katika kazi zao.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda