Akizindua zoezi hilo katika Kituo Cha shule ya Msingi Bigutu, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024, hivyo ametoa wito kwa Wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa wananchi waache kuchanganya kitambulisho Cha Mpiga Kura na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwamba kitambulisho hicho hakitatumika katika Uchaguzi huu badala yake kitatumika katika Uchaguzi Mkuu wa Mwakani.
Mwisho amesema ili uweze kumchagua Mwenyekiti wa mtaa poja na Wajumbe ni lazima ujiandikishe sasa.
Ewe Mwananchi nenda sasa ukajiandikishe Maendeleo ya mtaa wako!
Ijumaa 11 Oktoba 2024
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda