Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume akiongozana na timu yake, amepitia na kukagua miradi ya Afya katika Halmashauri za Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kukagua huduma za Afya jinsi zinavyotolewa.
Maeneo yaliyokaguliwa na kutolewa maelekezo ni utoaji wa huduma za Afya, Matumizi ya mifumo na fedha zinazoletwa na Serikali, Vifaa tiba na dawa, Miradi ya ujenzi, pamoja na uzingatiaji wa Sheria na taratibu za Matumizi ya Bima za Afya.
Akiongea katika kikao Cha majumuisho kilichofanyika katika Ukumbi wa Heriet katika Halmashauri ya Mji wa Bunda kikijumuisha timu zote za Menejimenti ya Afya (CHMT) katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mara, Dkt. Mfaume amesema ni lazima Idara za Afya zizingatie ushauri wote uliotolewa na Watalamu wa Afya kutoka OR-TAMISEMI waliyobaini wakati wa ukaguzi wa miradi.
Dkt. Mfaume amesema pia Uongozi Bora wenye ubunifu unasaidia pia kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wagonjwa. Mbali na kuupongeza Mkoa wa Mara kwa matumizi mazuri ya mfumo wa GoT-HoMis ametoa mkazo wa kuendelea kutumia vizuri mifumo hiyo ili kuepusha upotevu wa mapato ya Hospitali. Mwisho Dkt. Mfaume ameagiza umaliziaji wa miradi kwa wakati.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda