Mkutano Mkuu wa ALAT mkoa wa Mara umefanyika leo tarehe 28.05.2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda mara baada ya ziara ya kutembelea miradi iliyofanyika jana katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Akziungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa ALAT mkoa Mheshimiwa Daniel Komote amezipongeza Halmashauri zote za Mkoa wa Mara kwa maendeleo mazuri ya kukusanya mapato lakini pia amezielekeza kuekelea kumaliza mwaka kuongeza nguvu na jitihada za ukusanyaji ili kufikia malengo ya makadilio yao.
Sambamba na hilo, Mwenyekiti amezitaka Halmashauri kutenga asilimia 10 za mapato ya ndani na kuhakikisha wanazipeleka kwenye mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu. Na pia amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kurejesha fedha hizo ili na wengine wanufaike nazo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara ndugu Gerald Musabila Kusaya, amewapongeza wajumbe wote wa ALAT mkoa wa Mara kwa umoja na ushirikiano mzuri waliouonesha katika kipindi chote cha miaka mitano ambao wanalekea kumaliza muda wao.
Aidha katika kuelekea kipindi cha uchaguzi Mkuu, Katibu Tawala amewaomba wajumbe wa ALAT kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi. Na pia amewaomba wajumbe wa ALAT kuzisaidia Halmashauri zao kukusanya na kuongeza mapato.
Mkutano Mkuu wa leo ALAT ndio mkutano wa mwisho kwa wajumbe ambao ni madiwani wanaokwenda kumaliza kipindi chao cha miaka mitano mwezi ujao. Mwisho, Mwenyekiti amewatakia kila lakheri wajumbe ambao wataenda kutangaza tena nia kwa kipindi kijacho pindi harakati za uchaguzi zitakapoanza.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda