Leo Ijumaa ya tarehe 25.11.2022 Baraza la Biashara la Wilaya ya Bunda limewakutanisha Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa wafanya biashara wa Bunda TCCIA kujadiliana mambo kadha wa kadha ya kuijenga Wilaya ya Bunda na pia kufanya Mazingira wezeshi kwa Wafanyabiashara.
Mheshimiwa Nassari ameongelea kwa uzuri suala la Ulinzi na Usalama katika Wilaya ya Bunda kwamba iko vizuri Wafanyabiashara wafanye biashara kwa Amani kabisa.
Mheshimiwa Nassari amesisitiza sana ushirikiano na Uaminifu toka Wafanyabiashara hasa wanaopewa kazi na Serikali kuzifanyia kazi hizo wa Wakati kwani baadhi yao sio waaminifu wanapopewa kazi hawazifanyi kwa wakati na wengine kupandisha bei ya bidhaa zao kisa tu Serikali inataka kununua. Mheshimiwa Nassari amesema ushirikiano mzuri unaanza kwanza kwa Wafanyabiashara wenyewe na Kisha kwa wateja wao.
Aidha Mheshimiwa Nassari amewaambia Wafanyabiashara kwamba milango ya Ofisi yake ipo wazi muda wote pale wanapohitaji mashauriano yoyote kutoka Serikalini wanakaribishwa ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na Taasisi au Mamlaka, Kampuni au Mamlaka yoyote ambayo inaweza kuwafanikisha katika biashara zao.
Kwa upande wa Wakurugenzi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda amesema dai la ushuru wa Malazi la 10% ni Kubwa kama wanavyodai Wafanyabiashara, Mkurugenzi amesema ushuru huo upo kwa mujibu wa Sheria ambapo mwanzo ilikua asilimia 20 lakini kwa busara Bunge likapunguza na kuwa asilimia 10.
Wafanyabiashara pia walihoji juu ya Halmashauri kufanya biashara, Mkurugenzi alisema kuwa ni kweli Halmashauri inakiwanda Cha Tofali kama ilivyo kwa baadhi ya Halmashauri nyingine. Amesema kuwa Halmashauri iliamua kuanzisha kiwanda hicho kutokana na changamoto za ubora wa tofali zinazozalishwa na baadhi ya Wafanyabiashara na changamoto zilizojitokeza Wakati wa ujenzi wa Madarasa ya UVIKO zaidi ni kupunguza gharama.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Mkwazu aliongeza kusema kuwa Halmashauri ziliamua kufuata bidhaa za ujenzi viwandani kwasababu Wafanyabiashara wetu wanapandisha bei na wanakataa kupeleka biadhaa kwa baadhi ya vijiji vyake na wengine kuchelewesha bidhaa hizo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda