Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Kanali Evans Alfred Mtambi aipongeza Halmashauri ya Mjiwa Bunda kwa kuibuka na Hati safi ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa Miaka mitano mfululizo.
"Kwenye Halmashauri nyingine nilikokupita nilikua nakuta hoja ishirini na.., tisini na..nyingi kweli kweli, lakini hapa nimekutana na hoja chini ya ishirii na kimsingi 12 tu ndio zinazoendelea hongereni sana."
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri pia kuwa na maagizo matatu tu ya Kamati ya Bunge huku agizo moja likiwa tayari limeshatekelezwa. Katika hili ameitaka Menejimenti kuhakikisha wanafanyia kazi maagizo yote ya Kamati za Bunge.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameielekeza Baraza la Madiwani kushirikiana na Menejimenti kuibua vyanzo vipya vya mapato, kuimarisha usimamizi wa vyanzo vilivyopo, na kufanya upembuzi wa kina kubaini haki na stahiki za Halmashauri zitokana na shughuli za Utalii katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mwisho Mheshimiwa Mtambi amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa zinapelekwa benki, Halmashauri kuendelea kutengeza fedha za asilimia kumi za mikopo ya Wanawake vijana na watu wenye ulemavu lakini pia kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa wote wanaosababisha hoja.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyoge alieleza hali ya usalama katika Wilaya ya Bunda kwamba ni shwari. Mkuu wa wilaya alieleza hali ya tembo kuvamia makazi ya wananchi kutokana na kutafuta chakula ambacho ni mazao ya wananchi ambapo ofisi yake ilifanikiwa kukaa na uongozi wa wananchi hao na kuweka mikakati ya kuwazuia wanyama hao.
Mhe. Kaminyoge ameeleza pia kuwa Wilaya inajitahidi kuhamasisha wazazi kuchangia chakula shuleni na watoto kupata chakula shuleni, pia ameeleza zoezi la kukarabati wa miundombinu chakavu kuwa linaendelea katika sekta mbalimbali za serikali.
Wakati akitoa salamu zake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda Ndg. Mayaya Ibrahimu Magese ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kuendelea kufanya vizuri katika utendaji wa kila siku kuwahudumia wananchi, kupata Hati safi na kutekeleza vema ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda