UTANGULIZI
Halmashauri ya Mji wa Bunda ni Miongoni mwa Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara. Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024, Halmashauri ya Mji wa Bunda imekimbiza Mwenge leo Jumamos tarehe 03.08.2024 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Uwapo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa Kilometa 94 chini ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava. Mwenge wa Uhuru Umezindua, kuweka jiwe la Msingi na kutembelea Miradi 10.
MCHANGANUO WA MIRADI
Matukio mbalimbali yaliyotokea katika miradi ni kama ifuatavyo:
MIRADI ILIYOZINDULIWA
Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara. Mradi unathamani ya shilingi 100,420,815.00. Unapatikana Kata ya Bunda stoo. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge amesema mradi ni mzuri na amekubali kuweka jiwe la msingi
Hotel ya Golden Peak (Golden Peak Hotel). Mradi unathamani ya shilingi 209,000,000.00 Hotel hii ni mali ya mtu binafsi. Katika kutambua mchango wa Sekta binafsi, Serikali imeona ni vema mradi huu ukazinduliwa na Mwenge wa Uhuru. Kiongozi wa Mbio za Mwenge amekubali kufungua Mradi.
MIRADI ILIYOWEKEWA JIWE LA MSINGI
Zahanati ya Ligamba. Mradi huu umeenzishwa kwa nguvu za wananchi na baadae kushikwa mkono na Serikali kwa shilingi milioni 50. Jumla ya thamani ya mradi hadi sasa ni shilingi 53,390,800.00 Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kuwekanjiwe la msingi na kupongeza juhudi za wananchi kuanzisha ujenzi.
Ujenzi wa Bweni la Watoto wenye mahitaji maalum. Mradi unathamani ya shilingi 160,000,000.00 ikiwa milioni 130 kutoka Serikali Kuu na milioni 30 kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekataa kuweka jiwe la msingi kutokana na kuwa na mashaka na gharama za mradi zilizotumika na zinazohitajika kukamilisha mradi.
Ujenzi wa Madarasa sita na matundu nane ya vyoo. Mradi umejengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu wenye thamani ya shilingi 168,000,000.00. Mradi umegfikia hatu ya ukamilishaji. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kuweka jiwe la msingi kuutaka uongozi kuendelea kusimamia vizuri mradi ukamilike kwa wakati.
Ujenzi wa Mradi wa kuchakata maji taka Bunda Mjini. Mradi unathamani ya shilingi 1,728,019,700.00. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kuweka jiwe la msingi ujenzi uendelee.
Ujenzi wa Daraja la Bigutu – Nyasana. Mradi unathamani ya shilingi 232,970,000.00 Mradi upo katika kata ya Bunda stoo. Daraja hili limerahisisha shughuli za kiuchumi ya Wananchi wa Kata ya Kabasa na Bunda stoo. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kuweka jiwe la msingi.
MIRADI ILIYOTEMBELEA
Jengo la Radiolojia. Mradi huu ulizinduliwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023 hivyo Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zimeutembelea kutazama uendelevu wa mradi. Mradi upo katika Kituo cha Afya Manyamanyama. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kutembelea mradi
Kikundi cha Vijana Kazi Kazi (Kazi kazi Group). Kikundi kinajihusisha na Uuzaji wa nguo za Mitumba. Kikundi kinamtaji wa Shilingi milioni 2,900,000.00, kati ya hiyo fedha shilingi 2,000,000.00 walipataka kutoka katika mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kutembelea kikundi.
Mradi wa Mazingira katika shule ya sekondari Sazira. Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ulitembelea mradi wa Mazingira katika shule ya sekondari Sazira na kupata taarifa ya Upandaji miti kuanzi Julai 2023 hhadi Julai 2024 ambapo Halmashauri imefanikiwa kupanda miti 395,284.
Lakini pia Mwenge wa Uhuru umepanda miti 50 na kugawa miti 1000 kwa wananchi wa eneo hilo katika shule hiyo. Maoni ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amekubali kutembelea mradi na kkupanda miti.
Mwisho Mwenge wa Uhuru ulielekea katika eneo la Mkesha ambapo ulikagua Kongamano/Mdahalo wa Vijana, Banda ya Ujasiliamali, Uchaguzi na Baadae kusoma Risala ya Utii.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda