Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe. Michael Kweka amewapongeza wananchi wa Nyatwali kwa kumchagua Diwani makini mwenye Upendo na kuwajali wananchi wake.
Mwenyekiti amesema kuwa, Mheshimiwa Diwani wa Nyatwali amewapambania sana wananchi wake toka jambo lilipoanza hadi kufikia sasa malipo yalipokamilika.
Aidha Mheshimiwa Mwenyekiti amewataka wananchi hao kuwa makini na fedha watakazolipwa kuzitumia vizuri kujenga nyumba sehemu watakayohamia kuliko kufanyia starehe.
"Halmashauri ya Mji wa Bunda Bado ina Maeneo mengi ambayo yapo wazi mfano Kata ya Sazira, Mcharo, Guta na Wariku hivyo nawaomba msihame Halmashauri yetu bali msogee katika Maeneo hayo." Mhe. Kweka
"Mimi Mwenyekiti wenu niko pamoja na nyie mkihitaji ushauri wowote nawakaribisha muda wowote mje tuongee kuijenga Bunda yetu" amesema Mheshimiwa Kweka
#kaziiendeleee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda