Kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha katika Maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bunda, kumeibuka ugonjwa wa kutapika na kuharisha katika Kijiji cha Mekomariro.
Kamati ya Afya ya Wilaya chini ya Mwenyekiti Salum Mtelela Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, imekaa kikao Cha dharura kujadili namna gani ya kupambana na mlipuko huo.
Baadhi ya sababu zilizobainika kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni wananchi kutozingatia matumizi sahihi ya vyoo na asilimia kubwa ya Kaya nyingi kuonekana hazina vyoo, imebainika pia wananchi wengi wanatumia maji ambayo si safi na salama kutoka katika mabwawa yaliyotuhama maji.
Kufuatia sababu hizo kikao kimeazimia Uongozi wa Kata na Wilaya kwa ujumla kuhakikisha wananchi wanajenga vyoo hadi kufikia tarehe 10.01.2025 na kufuata matumizi sahihi ya vyoo.
Kikao kimeazimia kusitisha mikusanyiko isiyokua ya lazima katika Kijiji Cha Mekomariro na kuzuia huduma ya chakula katika misiba, minada na migahawa kuanzia Leo tarehe 04 mwezi wa kwanza 2025.
Aidha, kikao kimeelekeza Mamlaka ya Maji kuhakikisha inaboresha huduma ya Maji katika Kata hiyo na kuhakikisha wananchunguza na kutibu vyanzo Rasmi vya maji vinavyotumiwa na wakazi wa eneo hilo.
Mwisho, Kikao kimeelekeza Viongozi wa Maeneo hayo kuendelea kutoa elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira mara kwa mara.
Katibu Tawala ametoa maelekezo kwa Wananchi wote wa Bunda kuchukua tahadhari kwa kuzingatia misingi ya Usafi wa Mazingira na Vyakula ili kuepuka ugonjwa huo.
Jumamosi 04, Januari 2024.
Afya kwanza.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda