Mhandisi wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini Wilaya ya Bunda Eng. Baraka Mkuya amesema kwa mwaka wa fedha huu 2023/2024 TARURA imeidhishiwa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 2 na hadi sasa wameshapokea shilingi milioni 137.5 sawa na asilimia 6.6.
Mhandisi amesema mradi unaoendelea sasa ni mradi kiporo wa Mwaka wa fedha 2023 wa barabara zinazoelekea Hospitali ya Halmashauri ya Mji pamoja na Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Aidha Mhandisi Mkuya ameeleza kwamba kwa mwaka huu wa fedha TARURA inavyanzo Vitatu vya fedha ambavyo ni Matengenezo kutoka mfuko wa barabara, Tozo na fedha za Jimbo. Fedha zote hizi zitatekeleza miradi mbalimbali ya barabara katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Akijibu hoja za Wajumbe wa Baraza Mhandisi Baraka amesema miradi yote iliyopangwa katika bajeti itatekelezwa na ile itakayobadilishwa kwa makubaliano ya pande zote mbili itafanyika hivyo kulingana na umuhimu wa barabara hizo zikiwemo barabara za kuelekea shule mbili mpya za Msingi Azimio Nyasura na Bunda stoo.
Waheshimiwa Madiwani wamepongeza kazi nzuri zinazofanywa na ofisi hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda