Leo tarehe 19.08.2024 Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Mji wa Bunda imekutana kujadili utekelezaji wa Afua za Lishe katika kipindi Cha Robo ya Nne 2023/2024 chini ya Mwenyekiti Kaimu Mkurugenzi Bi. Adelina Mfikwa.
Kamati imepitia Afua Moja baada ya nyingine kuangalia mafanikio na changamoto zilizojitikeza wakati wa Utekelezaji wake na kutafuta suluhisho ya changamoto hizo.
Aidha Kikao kimeazimia Idara na Vitengo vinavyohusika na utekelezaji wa Afua za Lishe kuendelea kutoa elimu kwa wazazi kutambua umuhimu wa Lishe kwa wanafunzi na hivyo kuendelea kuwahamasisha kuchangia Chakula kwaajili ya watoto pindi wanapokua shuleni.
Kuendelea kuzihamasisha shule zenye mashamba kutumia mashamba hayo kuzalisha chakula kwa manufaa ya wanafunzi wa shule husika. Pia shule kutumia Vyakula vyenye virutubisho lishe kwa matokeo chanya kwa wanafunzi.
#kaziiendeleee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda