Kamati ya ALAT Mkoa wa Mara ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Daniel Komote imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda leo tarehe 27.05.2025.
Katika ziara hiyo wajumbe wameridhishwa na ubora wa miradi waliyoikagua na kupongeza uongozi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo. Aidha Kamati imepongeza Halmashauri kwa kutoa fedha za mapato ya ndani kujenga Maabara ya sayansi katika shule ya sekondari Paul Jones.
Kamati imeishukuru Serikali kwa kuleta fedha za kutosha za miradi katika Halmashauri ya Mji wa Bunda. Kwa upande mwingine, Kamati imewapongeza Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo kwa kuibua na kuanzisha miradi kisha Serikali kuunga mkono.
Katika ujenzi wa Zahanati ya Kitaramaka, Kamati imeunga mkono juhudi za Wananchi na Serikali kwa kuchangia kiasi cha Shilingi laki tano kwaajili ya kuongezea palipo na mapungufu.
Jumla miradi minne (4) yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3 imetembelewa na Kamati ya ALAT Mkoa wa Mara ambayo ni Ujenzi wa Maabara shule ya sekondari Paul Jones, Ujenzi wa Zahati ya Kitaramaka, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyasura na Ujenzi wa Uzio, Kantini na stoo katika Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda