Halmashauri ya Mji wa Bunda imeandaa Hafla fupi ya kuzipongeza shule za Msingi ambazo zimefanya vizuri katika Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la Nne na darasa la saba mwaka 2024.
Hafla hiyo jmefanyika leo tarehe 09 Juni 2025 katika ukumbi wa Heriet Bunda ambapo Mkuu wa Wilaya Mhe. Aswege Enock Kaminyoge alikua Mgeni rasmi.
Kabla ya kugawa Tuzo, Mgeni rasmi Mhe. Aswege Kaminyoge alisema ili ufaulu uongezeke na Halmashauri iendelee kufanya vizuri ni lazima Halmashauri isimamie na kuzingatia stahiki na maslahi ya Walimu kwa wakati, lazima motisha izidi kutolewa kwa wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vizuri kama pongezi na kutia hamasa ya kuendelea kufanya vizuri.
DC Kaminyoge ameongeza kusema kuwa, upimaji wa wanafunzi ni lazima uwe sawa kwa shule binafsi na shule za Serikali ili ushindani uwe wa kutosha kwa wanafunzi wote, ni lazima suala la lishe kwa wanafunzi lizingatiwe hasa wanafunzi kula shuleni ambapo ameelekeza kata na mitaa kufanya vikao vya kukubaliana kuchangia chakula kwaajili ya wanafunzi shuleni. Na mwisho amesisitiza kuendelea kufanya vikao vya tathimini ili kubaini mapungufu yaliyobainika ili yafanyiwe kazi na kupanga mikakati mipya.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ndg. Juma Haji Juma alisema Halmashauri imekua ikitoa motisha kwa walimu na kufanya Tathimini ya Upimaji wa darasa la saba na darasa la nne na kwamba huu ni msimu wa Pili toka zoezi hili lianze.
Aidha Mkurugenzi alisoma alisoma matokeo ya shule jinsi zilizvyofanya kwa darasa la saba na darasa la nne ambapo alisema kuwa darasa la saba wamefaulu kwa asilimia 72.1 na darasala nne wamefaulu kwa asilimia 73. Mwisho Mkurugenzi amemhakikishia Mgeni rasmi ya kwamba atasimamia maelekezo yote aliyoyatoa na kuhakikisha yanatekelezwa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda