Siku ya Leo ilikua nzuri sana kwa wakazi wa Kata ya Balili ambapo timu ya Watalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ilitia nanga kusikiliza na kutatua kero zao.
Akiongoza Mkutano huo Diwani wa Kata ya Balili Mheshimiwa Tamka Thomas, amewaongoza wananchi kueleza kero zinazowakabili katika Maeneo yao. Baadhi ya kero walizoeleza ni:
Wanyama wakali kama Fisi, Tembo na Nyani kuvamia makazi yao, eneo la kunyweshea mifugo yao, ubovu wa barabara za Mitaa, uhaba mtandao wa maji ya bomba, mifugo kuzurura na kuzagaa hovyo, eneo la wazi lililotengwa kwaajili ya Soko, dimbwi la maji linalohatarisha maisha ya watoto pamoja ukosefu wa umeme kwa baadhi ya Maeneo.
Watalamu kutoka Halmashauri na Taasisi wakiongozwa na Mratibu wa Malalamiko Mwl. Arende aliwaongoza kujibu hoja za wananchi.
Kusuhu Wanyamapori wakali na waharifu Afisa Wanyamapori Bi. Stella Masakilija aliwaeleza wananchi kwamba Halmashauri ipo kwenye mikakati na TAWA ya kuona namna ya kuwadhibiti wanyama hao kwani kwa sasa inaonekana kuwa wengi sana.
Kuhusu Maji Afisa usambazi maji Mhandisi Vumi amewaelewa wananchi kuwa tayari BUWSSA ipo kwenye mchakato wa kusambaza huduma ya Maji ambapo wakazi wote wa Balili watapata huduma ya Maji safi na salama.
Kuhusu mifugo inayozurura hovyo Afisa Mifugo Bwn. Kaduri ameelimisha wananchi juu ya kufuga mifugo yao na kuifungia katika eneo Moja kwani kuwaacha ni kuleta kero kwa wengine na kuharibu mazao ya wengine.
Kwa upande wa barabara Mhandisi Kalomo amesema baadhi ya Barabara zipo kwenye Mpango na Bajeti ya Mwaka 2024/2025 na kuanzia mwezi wa saba zitaanza kutengenezwa na kwa zile ambazo hazimo basi TARURA itashirikiana na Viongozi wa mitaa kutembelea na kubaini mahitaji ya hizo Barabara.
Kuhusu eneo la wazi lilotengwa kwaajili ya Soko, Afisa Ardhi na Mipangomiji Richard Pungu amesema kwa kushirikiana na Viongozi wa mtaa huo wanaolijua vizuri eneo hilo linalosemekana kuvamiwa watalifuatilia kufahamu ukubwa wake pamoja na nyaraka zilizopo zinazoonesha umiliki wa eneo hilo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda