"Malipo ya fidia ya wananchi wa Nyatwali kuhama kupisha eneo kwaajili ya Hifadhi yamefika. Fedha hizo zimeshawekwa katika Akaunti ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kinachofuata sasa ni malipo. Kila Mwananchi ahakikishe Akaunti yake ya Benki inafanya kazi na kama haifanyi kazi nenda kaihuishe na kwa wasiokua na Akaunti mfungue sasa. Benki zote zitaweka Kambi hapa kwaajili ya kuwasaidia. Amesema DC. Dkt. Anney
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameongeza kusema "Malipo yatafanyika kwa Wananchi wote waliofanyiwa tathimini. Kila mmoja atalipwa kiasi alichofanyiwa Uthamini."
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa angalizo kwa wananchi wenye migogoro kumaliza migogoro yao mapema kabla ya kufanya malipo kinyume na hapo malipo hayatafanyika.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema pindi malipo yatakapokamilika, Wananchi watatakiwa kuondoka katika Kata hiyo ndani ya Siku 90.
Kwa upande mwingine DC Anney amewataka kutofanya uharibifu wa aina yoyote kwa kipindi hiki kutokata miti wala kubomoa nyuma bila kibali.
Haya yote yamejiri Leo katika Kikao kilichofanyika Kata ya Nyatwali kwa lengo kuwafahamisha Wananchi wa Nyatwali suala hili la fidia.
#kaziiendeleee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda