Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda Ndg. Mayaya Abraham Magese amewapongeza Watumishi wa Wilaya ya Bunda kwa namna wanavyosimamia na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
"Nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, amekua akipokea na kutekeleza maelekezo ya Chama, kusimamia miradi na kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati." Amesema Mwenyekiti Ndg. Mayaya Abraham Magese
"Niwapongeze pia Wakurugenzi na Watendaji wao kwa namna ambavyo mnatekeleza miradi ya maendeleo na kusimamia vizuri fedha zinazoletwa na Serikali." Mwenyekiti Mayaya
Mwisho Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM pamoja na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wamepokea na kupitisha Taarifa ya Serikali kwa kipindi Cha mwezi Julai - Disemba.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda