Mwenyekiti wa Baraza Mheshimiwa Malongo Mashimo ameongoza Mkutano wa Baraza kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango na Bajeti wa Mwaka 2025/2026.
Bajeti hii kabla ya kuingia kwenye Baraza ilijadiliwa na Kamati husika Kamati ya Uchumi Elimu na Afya, Kamati ya Mipangomjini na Mazingira na Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri na kufanya marekebisho ambayo yalisubiri Mkutano wa Baraza kuyapitisha.
Baada ya wajumbe kujadili na kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana na wananchi wa Bunda wanapata huduma inayoridhisha, Mwenyekiti alihoji Baraza kama linakubali kupitisha kupitisha Bajeti hiyo.
Wajumbe wote kwa sauti ya pamoja walikubali kupitisha Mpango na Bajeti wa Mwaka ujao wa fedha 2025/2026 wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32.2 pamoja na marekebisho yake.
#kaziiendeleee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda