Kikao cha timu kutoka Halmashauri ya Mji wa Bunda Waheshimiwa Madiwani na Watalamu wakibadilishana uzoefu wa kazi na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Ziara hii imelenga kujifunza mbinu mpya za uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda katika kukusanya Mapato, Usafi wa Mazingira, kuboresha mahusiano, ushirikiano na kuwahudumia vema wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Aidha baada ya Kikao hicho timu ilipata nafasi ya kutembelea baadhi ya vitega uchumi vya Halmashauri ikiwemo kiwanda Cha kutengeneza tofali, Soko la madini na Vibanda vya kisasa vilivyojengwa kwaajili ya wafanyabiashara.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda