|
UJENZI WA OFISI YA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA MJI WA BUNDA
Halmashauri katika mwaka wa fedha 2017/2018 na 2016/2017 imepokea jumla ya Tshs 2,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri. Mpaka sasa ujenzi unaendelea uko hatua ya msingi. Mkandarasi ni SUMA JKT chini ya usimamizi wa wakala wa majengo Tanzania. Mkataba wa ujenzi ni wa Tshs 3,162,466,563 mpaka kufikia mwezi Mei malipo yaliyofanyika ni Tshs 831,772,028 ambapo mkandarasi amelipwa Tshs 722,024,329.50 na mtaalamu mshauri Tshs 109,747,698. Mkataba wa utekelezaji mradi ni miezi 10. |
|||||||||
|
KITUO CHA AFYA CHA BUNDA
Halmashauri ilipokea Tshs 500,000,000 kwa ajili ya uboreshaji kituo cha Afya Bunda kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji, maabara, wodi ya mama na mtoto, nyumba ya mtumishi na jengo la kuhifadhia maiti. Mpaka mwezi Mei jumla ya Tshs 487,000,000 zimetumika. Majengo yote yamejengwa,kuezekwa, kupigwa lipu, kuwekewa madirisha na milango, kupakwa ranging, kuwekewa vigae na mfumo wa maji na umeme umewekwa. Shimo za maji taka zimejengwa. Pamoja na kazi hizi choo cha nje cha ziada zimejengwa, uzio umejengwa na njia za kupita wagonjwa zimejengwa. Kazi hii inafanyika kwa kutumia mafundi tofauti kwa kila jengo chini ya utaratibu wa ''force account'' kulingana na maelekezo ya serikali katika kutekeleza miradi hii |
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda