Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mji wa Bunda Ndg. Michael Kweka akifungua Baraza la Halmashauri robo ya kwanza 2021/2022 kujadili ajenda 11 kama zilivyopitishwa na Waheshimiwa Madiwani.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndg. Salum Mtelela, akitoa maelekezo ya Serikali katika Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda uku akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali na ushirikiano kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani katika kusimamia shughuli za maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Bunda. Aiadha ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watendaji kushirikiana kwa pamoja kutokameza mimba mashuleni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel Mkongo akitoa ufafanuzi na ushauri kwa baadhi ya hoja zilizokuwa zikiibuka katika mkutano wa Baraza la Halmashauri la robo ya kwanza.
Mheshimiwa Robert Chacha Maboto, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini akitoa ushauri kwa Watendaji kushirikiana na waheshimiwa madiwani katika kutekeleza na kusimimamia miradi inayotekelezwa na Serikali chini ya Chama cha Mapinduzi uku akiwaomba Waheshimiwa Madiwani kutokua vikwazo kwa wananchi kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa madarasa unaoendelea chini ya ufadhili wa Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko - 19
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe. Mathayo Machiru akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo kwa Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano wa baraza.
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifatiilia kwa ukaribu Baraza la robo ya kwanza 2021/2022
Mheshimiwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda akifunga Mkutano wa Baraza la Halmashauri kwa robo ya kwanza uku akiwashukuru Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na wageni waalikwa kwa mahudhurio mazuri na kufungua dirisha la ushauri katika masuala ya kuijenga Halmashauri yetu.
Mwonekano wa Baraza la Halmashauri wakati mkutano ukiendelea
Baadhi wa wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wageni waalikwa wakifatilia kwa ukaribu Mkutano wa Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wageni waalikwa wakifatilia kwa ukaribu Mkutano wa Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda
Meneja TARURA Ndg. Kalomo akieleza hali ya utetekelezaji na ukarabati wa barabara mbalimbali katika Halmashauri ya Mji wa Bunda. Aidha Waheshimiwa Madiwani wamemshauri Meneja Tarura kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani kubaini barabara zenye changamoto zaidi kupewa kipaumbele kukarabatiwa na kujengwa upya.
Kaimu meneja Buwsa akijibu maswali kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani uku akieleza kuwa changamoto ya maji inayojitokeza sasaivi ni kutokana na mabomba mengi kukatwa katika ujenzi wa barabara ya Bunda - Serengeti unaoendelea hivi sasa, hata hivyo changamoto hizo zimeshaanza kupatiwa ufumbuzi na muda si mrefu maji yatatoka kama kawaida.
Meneja BUWASA Ndg. Mfungo, akielezea miradi ya maji inayotekelezwa sasa katika mitaa ambayo hapo awali ilikua vijiji ikiwa ni pamoja na mradi uliotengewa fedha na Serikali shilingi milioni 500 kupeleka maji Mtaa wa Bitaraguru kata ya Kabasa. Ndg. Mfungo amesema mradi huo upo kwenye hatua za mwisho kufanyiwa kazi na kuongeza kuwa fedha hizo zitasadia kuongeza pampu ya pili ili kuhakikisha wakazi wa Bitaraguru wanapata maji ya uhakika wakati wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda akiendelea kutoa msisitizo kwa baadhi ya mambo katika Mkutano.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda