Jumatano 09.08.2023
Balozi wa pamba nchini Tanzania Mhe. Aggrey Mwanri amefanya ziara yake katika Wilaya ya Bunda kwa kuzikutanisha Halmashauri zote mbili huku akitoa semina kwa Watendaji kata , Mitaa, Vijiji, Maafisa Ugani, wawakilishi wa AMCOS, wawakilishi wa makampuni ya kilimo na wataalum wa kilimo toka Halmashauri zote mbili za Bunda juu ya kuongeza tija katika kilimo cha pamba.
Awali, mwenyeji wake Ndg. Salum Mtelela Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda kwa niaba ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, alitoa pongeza kwa Barozi wa pamba kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa Wakulima wa pamba ambayo inawafanya kuongeza tija katika kilimo cha pamba. Katibu Tawala alitoa wito wa wajumbe wa Kikao kusikiliza na kufuata mafundisho ya barozi ili kufikia malengo ya Serikali ambayo kama Wilaya imepangiwa kutimiza katika uzalishaji wa pamba.
Mhe. Aggrey Mwanri amesisitiza uanzishwaji wa mashamba darasa katika kipindi hiki ambacho wakulima wengi wa pamba wapo likizo na wanaendelea na uuzaji wa pamba katika masoko.
Aidha, Balozi amesema kuwa mashamba darasa hayo yanatakiwa kuanzishwa ifikapo tarehe 15.08.2023 ili kuwapa elimu bora wakulima kabla ya kuanza kilimo na hii itawasaidia sana wakulima kuweza kupata mazao bora kwani wataanza kulima kwa wakati wakiwa na elimu sahihi.
Hata hivyo, Balozi wa pamba nchini Tanzania amesisitiza matumizi bora ya pembejeo za kilimo ilkiwemo samadi na mbegu mbora za kilimo pia sumu za kuulia wadudu, ambapo pia ameeleza mbinu bora ya kulima (60:30), kuandaa mashamba mapema na jinsi gani ya kuvuna pamba na kuhifadhii ili iwezee kua bora na yenye ushindani.
Kwa upande mwingine Balozi wa pamba ametoa takwimu za kupanda na kushuka kwa bei ya pamba katika soko ambapo amesema wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO (Covid -19) bei ya pamba kwa kilo moja ilifika shiling 2,400/- lakini baada ya Covid -19 bei ya pamba ilishuka hadi kufikia Tsh. 1,060/- hii ni kwa sababu ya ongezeko la nchi ambazo zinalima pamba kuanza kuuza tena pamba katika soko la dunia.
Lengo la Serikali ni kufikia uzalishaji wa Tani milioni moja na kuwa kinara wa uzalishaji Afrika.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda