Jioni ya Leo imekua siku tulivu kabisa na yenye matumaini kwa wananchi wa Bunda hasa wale wasiokua na uwezo wa kupata futari ambapo BAKWATA Wilaya ya Bunda imeandaa futari na kualika watu mbalimbali toka dini mbalimbali kushiriki futari hiyo.
Mgeni rasmi katika futari hiyo alikua Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dkt. Vicent Anney. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amelishukuru Baraza la Waislamu kwa kuandaa futari hii na kuweza kushirikisha watu mbalimbali. Dkt. Anney amesema dini ndio inayotukutanisha watu wa aina mbalimbali na funga inatufanyabkuwa karibu na Mwenyezi Mungu kwa ni kipindi ambacho ni Cha sala na toba.
Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametumia fursa hiyo kuongea na walioshiriki kuhusu kushirikiana kubaini wezi hasa wanaoiba taa za barabarani. Mkuu wa Wilaya amesema Serikali inamapenzi mema na wananchi wake na ndio maana inaboresha Miundombinu Kila siku, lakini kumeibuka kikundi Cha watu wasiopenda Maendeleo na kuharibu Miundombinu ya Taa za barabarani. Hivyo amewataka wananchi wote wa Bunda kushiriki kuwabaini na kuwakamata wezi hao.
Awali akiwakaribisha na kuwashukuru wageni wote walioshiriki futari Shekh wa Wilaya ya Bunda Abuubakar Bin Ally amesema, lengo la futari ya pamoja ni kuwaunganisha wananchi pamoja na Viongozi wao, kujenga mahusiano mazuri na kuzidi kutoa ushirikiano kwa Viongozi waliopo madarakani.
Shekh Abuubakar ameongeza kusema Vitabu vya dini vinatukumbusha kujenga mahusiano kwanza na Mungu, Pili kujenga mahusiano na wewe mwenyewe na mwisho kujenga mahusiano na Jirani yako.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda