Akiwasilisha Bajeti ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini Mhandisi Ahimidiwe Kiluswa mbele ya Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda amesema TARURA imetenga kiasi Cha shilingi Bilioni 2.098 kwaajili ya Matengenezo, Maboresho na Ukarabati wa barabara za Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mhandisi Kiluswa amesema Bajeti hii imefata vipaumbele vya Waheshimiwa Madiwani walivyowasilisha kutoka katika maeneo yao na ameongeza kusema kuwa Matengenezo yatakayokwenda kufanyika yatakwenda kuondoa changamoto na kero za wananchi juu ya barabara zilizopo katika Maeneo yao.
Awali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza Mhe. Michael Kweka, Waheshimiwa Madiwani walieleza changamoto za barabara zilizopoto katika Kata zao na kumtaka Meneja wa TARURA kuzizingatia katika bajeti hiyo.
Akifunga Mkutano wa Baraza Mheshimiwa Mwenyekiti amesema Milango ya Ofisi ya TARURA iko wazi na pindi Waheshimiwa Madiwani watakapotaka kubadilisha vipaumbele kulingana na umuhimu wa barabara basi wanaruhusiwa kufika Ofisini kwa Meneja kufanya majadiliano.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Vicent Anney amelitaka Baraza kuendelea kumuunga mkono na kumpatia ushirikiano wa kutosha Menejea mpya wa TARURA ili wote kwa pamoja waweze kuondoa changamoto za barabara zilizopoto katika maeneo yao.
Mwisho Mhandisi Ahimidiwe Kiluswa ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuleta fedha za kuboresha Miundombinu ya Barabara kuondoa changamoto kwa wananchi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda