Leo Jumatano 04.10.2023 Benki ya NMB imeikabidhi Halmashauri ya Mji wa Bunda Madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 12.
Akitoa neno la shukrani Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Dkt. Vicent Anney ameipongeza benki ya NMB kwa madawati waliyotoa ikiwa ni moja ya jitihada zinazofanywa na Serikali kuondoa upungufu wadawati katika shule za Msingi.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka benki ya NMB kuendelea kujitoa zaidi na ikiwezekana kuongeza idadi ya madawati ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa wilaya nzima.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewataka Waheshimiwa Madiwani kuandaa utaratibu mzuri utaowafanya wazazi na walezi Bunda nzima kuchangia madawati walau dawati moja kwa wazazi watatu.
Awali, Bwn. William Makoresho Mkuu anayesimamaia biashara za Serikali na Binafsi katika bemki ya NMB alisema, benki ya NMB ipo katika muendeleo wa kutoa huduma kwa jamii hususani katika sekta ya Elimu kwa kuchangia uhitaji wa madawati. Aidha Bwn. William amesema benki itaedelea kutenga bajeti zaidi kwaajili ya kuendelea kutoa huduma hizo.
Mwisho Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mheshimiwa Michael Kweka, Diwaniwa Kata ya Nyasura na Diwani wa kata ya Bunda Mjini pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda walitoa shukrani kwa benki ya NMB kwa kukabidhi madawati hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yatawasaidia wanafunzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Tukio hilo la kukabidhi madawati limefanyika katika shule ya Msingi Nyasura.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda