Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Bunda (BUWSSA) Bi. Esther Gilyoma amelieleza Baraza miradi mikumbwa ambayo inatekelezwa na BUWSSA amesema:
Mradi Mkubwa wa chujio la Maji Nyabehu umefikia asilimia 99 na pindi utakapokamilika watamuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aje kuzindua.
Mradi wa Maji Manyamanyama Mugaja mradi umefikia Asilimia 81 ambapo kazi ya kulaza mabomba imekamilika, mita zimeshanunuliwa na sasa tenki la maji linaendelea kujengwa ambapo malengo ni kwamba wananchi watapata maji kabla ya Christmas.
Mradi wa Balili Kunzugu unaendelea kutekelezwa ambapo tayari zaidi ya kilomita 6 zimeshatandazwa bomba na kazi bado inaendelea kabla ya Christmas wananchi watafurahia maji safi.
Mkurugenzi amesema katika kupambana na upotevu wa maji, sasa watatoa shilingi Elfu 50 kwa yeyote atakayetoa taarifa za wizi wa maji.
Aidha Bi. Esther amesema wameandika andiko la bilioni 5 likihusisha maeneo yote ya Bunda Mji ambapo kama litafanikiwa basi kero ya maji itakwisha yote.
Mwisho Bi. Esther amesema hoja zote za Waheshimiwa Madiwani amezipokea na atazifanyia kazi kwani lengo lao ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda