Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney ametoa Onyo kali kwa Taasisi au Watu Binafsi wanaochukua Kadi za Benki za Watumishi wanaokopa kwao kinyume na taratibu za ukopeshaji.
Dkt. Anney Ameyasema hayo Leo wakati akiongea na Taasisi/Watu Binafsi wanaotoa huduma ya Mikopo ya fedha katika Ukumbi wa Ofisi yake.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema "Kufanya hivyo ni Utapeli na wengine wamekua wa wakiongeza Riba bila Utaratibu, wengine wanaongeza Mikopo baada ya Mkopo wa mteja kuisha tena bila Utaratibu. Mkuu wa Wilaya ameagiza tabia hizo kukoma.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameelekeza Taasisi au Watu Binafsi wanaokopesha ambao hawajasajiliwa kujisajili kabla hajaanza kufanya opareshi ya kukagua.
Sambamba na hilo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa Onyo kwa wanaowalaghai Wastaafu kwa kuwapa Mikopo isiyoeleweka na kuchukua fedha zao na pia amekataza kukamata Mali ya mteja bila kibali Cha Polisi.
Mwisho Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewaelekeza wafanyabiashara hao kufuata Utaratibu wa ukopeshaji uliotolewa na kwamba yeyote atakaekiuka atachukuliwa hatua za kisheria. Aidha amesema Mikopo yote lazima ihusishe salary slip ya mtumishi na mkataba uoneshe muda wa marejesho, makato pamoja na riba.
Kwa upande wao wafanyabiashara wamemshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kukaa pamoja nao kutoa elimu na kusikiliza kero zao ambapo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameahidi kuzifanyia kazi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda