Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kutekeleza vizuri miradi ya Elimu na Afya iliyoletwa na Serikali ya awamu ya sita.
Dkt. Anney amewaagiza Waheshimiwa Madiwani kufanya mikutano ya Hadhara kuwaeleza Wananchi kazi kubwa inayofanywa na Serikali kupitia utekelezaji wa miradi hiyo.
Mkuu wa Wilaya amewakumbusha Watendaji wa Halmashauri kutekeleza maagizo yanayotolewa na viongozi kwa wakati. Ameyasema hayo akinukuu baadhi ya maelekezo aliyoyatoa wakati wa ziara yake aliyoifanya katika katika Kata za Halmashauri ya Mji ikiwemo migogoro ya ardhi na uwekaji wa vifaa vya kutunzia taka maeneo ya stendi na biashara.
Dkt. Anney ameielekeza Halmashauri kufanyia kazi migogoro yote ya ardhi hasa iliyopo katika maeneo ya Taasisi kwa kulipa fidia wananchi waliohamishwa katika maeneo hayo akitolea mfano wa Eneo la EPZ, Shule ya Msingi Nyerere na Manyamanya.
Aidha, ameongeza kwa kuielekeza Halmashauri kushughulia madeni ya Wastaafu wote wanaodai pamoja na madeni ya wananchi walioshinda kesi mahakamani dhidi ya Halmashauri.
Kwa upande mwingine, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo ya kusikiliza malalamiko ya wananchi kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata na Halmashauri kuliko ili kupunguza kero zinazopelekwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Dkt. Naano ameelekeza kuwa kesi zinazokua ngumu barua iandikwe ya kuomba usaidizi katika ofisi yake.
Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuongeza umakini katika suala la ukusanyaji mapato ambapo kuna upotevu mkubwa hasa katika maeneo ya minada. Pia amekemea suala la wizi na kuitaka Menejimenti kuwafuatilia kwa umakini watumishi ambao sio waaminifu katika ofisi zao hasa katika masuala ya manunuzi.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameelekeza kuongeza umakini katika Kamati za ujenzi zinazochaguliwa kuliko kuwaachia kila kitu kwani wengine sio waaminifu.
Kwa upande mwingine, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa angalizo la kutenga maeneo ya michezo na starehe wakati wa upimaji. Katika hilo amelitaka sakata la ujenzi wa Kiwanja kwaajili ya timu ya Bunda Queens kufuata utaratibu wa kisheria.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda