Siku ya Leo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney ameweka jiwe la Msingi katika shule mpya ya Sekondari ya Bunda Mjini ikiwa ni Maandalizi ya Uzinduzi utakaofanyika hivi karibuni.
Katika tukio hilo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameishukuru Serikali kwa kuleta fedha zaidi ya shilingi milioni 580 kupitia mradi wa SEQUIP kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema ujenzi wa shule hiyo umesaidia sanai watoto wa Bunda stoo kutembea umbali mrefu kufuata Elimu na pia umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za jirani.
Mwisho Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewakumbusha wanafunzi waliofikisha miaka 18 na zaidi kujiandaa kujiandikisha kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa muda utakapofika yani tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda