Kufuatia sintofahamu ya mpaka wa kiutawala kati ya wananchi wa Mtaa wa Kiwasi na wananchi wa Kijiji cha Nyakiswa jambo lililopelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Mkuu wa Wilaya ya Butiama pamoja na Wataalamu wa Ardhi kutoka Wizarani na Halmashauri kuingilia kati na kuondoa sintofahamu hiyo kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Dkt. Vicent Anney pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Moses Kaegele wamesema hakuna haja ya kugombania mashamba kwasababu ya mpaka wa kiutawala uliopo. Wamefafanua kuwa mwananchi yeyote aliye na shamba kati ya pande hizo mbili za mpaka anaruhusiwa kuendelea na shughuli zake kwa kuzingatia sheria na taratibu za sehemu husika.
Viongozi hao wamesisitiza kuwa uwepo wa mpaka hauzuii shughuli za kilimo kuendelea kufanyika katika maeneo hayo.
Aidha, viongozi wamewaasa wananchi kulinda amani katika eneo hilo na pasitokee dalili ya uvunjifu wa amani.
Mwisho wananchi walielezwa kwamba Wataalamu kutoka Wizarani na Halmashauri zote za Mji wa Bunda na Butiama wamekuja kuonesha mipaka ya kiutawala iliyopo kwa mujibu wa ramani ya eneo hilo na pia wameaswa kuheshimu na kutambua mipaka hiyo ambayo kwa beacon zitawekwa.
Zoezi la utambuzi wa mpaka na kuwaonesha wajumbe wa Kamati uliendelea baada ya kikao kumalizika ukihusisha zoezi la kubainisha maeneo ya uwekaji Beacon.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda