Akilihutubia Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney amesema anataka kuona miradi yote ya ujenzi ndani ya Halmashauri mipya na inayokamilishwa iliyoletewa fedha na Serikali inakamilika kwa wakati na katika ubora unaotakiwa. Huku akiwaelekeza wahusika wa Miradi hiyo kufanya usimamizi wa kina na kuepusha mianya ya uhujumu wa Miradi hiyo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewaelekeza Wahandisi kufanya tathimini kwa Miradi mipya ambayo Halmashauri imeshapokea fedha ya utekelezaji kuangalia kama fedha hizo zinaweza kukamilisha mradi kabla ya kuanza ujenzi.
Kwa upande mwingine, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kujenga tabia ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi waliopo chini yao.
Mwisho Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewasisitiza Waheshimiwa Madiwani na Wajumbe wengi kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27.11.2024.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda