Usiku wa Ijumaa tarehe 29.09.2023 ulikua usiku murua kabisa na wenye furaha Watumishi wa shule ya sekondari Bunda ambapo iliandaliwa hafla mahususi ya kutambua jitihada, kupongezana na kupeana zawadi kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kuwafundisha wanafunzi na kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita mwaka 2023.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Ndg. Salum Mtelela Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda hakusita kutoa pongezi zake kwa Watumishi wote wa shule ya Sekondari Bunda kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuweza kuendeleza ufaulu mzuri kwa miaka mitatu mfululizo.
Katibu Tawala amewataka walimu kuendeleza nguvu na jutihada ili wazidi kufanya vizuri zaidi na kuendelea kuitangaza Halmashauri ya Mji wa Bunda na Wilaya ya Bunda kwa ujumla.
Aidha, Katibu Tawala ametoa ahadi ya zawadi toka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kiasi cha Shilingi laki nne na na Tisini na pia amewaahidi kuwapeleka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwemda kutalii na kuburudika kama alivyofanya kwa shule ya sekondari Sazira.
Awali Mkuu wa shule ya Sekondari Bunda Mwl. Charles Somba alisoma mafanikio makubwa ambayo shule imeweza kuyapata kwa takribani miaka mitatu mtawaliwa kama ifuatavyo:
Mwaka 2021 jumla ya wanafunzi waliofanya mtihami walikua 88 kati yao 73 walipata daraja la kwanza na 15 walipata daraja la pili shule ikashika nafasi ya pili Kimkoa na 21 Kitaifa.
Mwaka 2022 waliofanya mtihani walikua 115 kati yao waliopata daraja la kwanza ni 104, wanafunzi 10 daraja la pili na mmoja pekee alipata daraja la 3. Shule ilishika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya 15 Kitaifa.
Mwaka huu 2023 wanafunzi waliofanya mtihani walikua 126 kati yao wanafunzi 121 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 4 walipata daraja la pili na mwanafunzi mmoja pekee alipata daraja la tatu. Shule ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza Kimkoa na ya 19 Kitaifa.
Mwalimu Somba aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuwapongeza ikiwamo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, wadau wa Elimu kama Ndg. Alphayo Kidata, Ndg. Juma Makongoro na kuchimbiwa kisima cha maji safi kutoka Kanisa la AICT Dayosis ya Mara na Ukerewe chenye thamani ya shilingi milioni 30.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda