Katika muendelezo wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, leo ilikua zamu ya Kata ya GUTA ambapo wananchi wamewasilisha kero zao na kujibiwa na Watumishi wa Idara husika.
Kikao hiki kimefanyika chini ya Mwenyekiti Mhe. Kigho Nyakimoro Diwani wa Kata ya Guta kimekua kikao chenye mafanikio na matumaini kwa wakazi wa Guta ambapo hoja zilizowasiliwa na wachache zimewakilisha wananchi wengi wa eneo hilo. Watumishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wamepokea hoja na kuzijibu.
Kwa hoja ambazo Viongozi husika hawakuweza kufika katika Kikao kutokana na majukumu mengine ya kazi zikiwemo hoja zinazohusu huduma ya Maji, umeme, ardhi na Wanyamapori waharifu zimechukuliwa na kuahidi kuzifikisha kwa wahusika na Kisha majibu kurejeshwa kwa wananchi.
Mwisho Wananchi wameomba kikao hiki kurudiwa tena siku nyingine kikiwa na Viongozi wote wanaoguswa na hoja ili waweze kuzijibu na kutoa ufafanuzi wa hoja hizo ambapo Afisa anayeratibu malalamiko Mwl. Erasto Arende ameahidi kulifanyia kazi kwa kupanga tarehe na Kisha Mkutano utafanyika tena.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda