"Kwasasa wakati mchakato wa kuhamisha ukiendelea wanafunzi watafanyia mitihani katika shule wanazosoma sasa." Hayo ni majibu ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo wakati akijibu swali la Diwani wa Kata ya Nyatwali.
Mkurugenzi amesema zoezi ambalo lilikua muhimu la uthamini kwaajili ya fidia tayari limeshakamilika na vitabu vimeshaandaliwa na ni baadhi ya mambo yanasubiriwa na pindi yatakapokamilika basi kila kaya itaamua ni wapi watahamia.
Mkurugenzi ameongeza kusema kuwa kazi ya Halmashauri kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wizara ya OR-TAMISEMI itawahamisha wanafunzi hao kulingana na maeneo waliyohamia.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda