Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mwl. Said Ramadhani amefungua Mafunzo kwa Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Kata na kuwataka kuonesha uaminifu na utiifu wa kusimamia Sheria na taratibu za utoaji wa Mikopo kwa ngazi yao ili kutimiza azma ya Serikali kutoa Mikopo hiyo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
Kaimu Mkurugenzi amesema, Serikali imeamua kuleta mfumo mpya wa utoaji wa Mikopo kwasababu Awali udanganyifu ulikua mkubwa na kusababisha fedha nyingi za Serikali kupotea, hivyo miongozo iliyotolewa itasaidia kulinda fedha hizo na Sheria itachukua hatua kwa yeyote atakaekaidi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda