Alhamis 24.08.2023
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya Bunda chini ya Mwenyekiti Mhe. Mayaya Abraham Magese imefanya kikao cha Majumuisho na Viongozi wa Serikali juu ya ziara iliyofanyika katika majimbo yote matatu ya Mwibara, Bunda na Bunda Mjini.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2023.
Jumla ya miradi 39 yenye thamani ya shilingi bilioni 37.08 imetembelewa katika majimbo yote matatu. Miradi 12 katika jimbo la Mwibara, Miradi 10 jimbo la Bunda na Miradi 17 katika jimbo la Bunda Mjini.
Kamati imeipongeza Serikali kwa utekelezaji mzuri wa Ilani kwa kusimamia vizuri miradi na fedha zilizotolewa na Serikali chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Kamati imetoa mapendekezo, Ushauri na Maelekezo kwa Miradi ambayo ilibainika kuwa na mapungufu ili iweze kufanyiwa marekebisho na maboresho.
Serikali kupitia Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dkt. Vicent Anney imepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya siasa na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
Zaidi Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa yeye pamoja na Watendaji wake hawako tayari kuona miradi ya Serikali inahujumiwa, kuibiwa ama kutekelezwa chini ya kiwango.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda