Katika Kikao Cha Majumuisho ya ziara ya Siku Tatu ya Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bunda chini ya Mwenyekiti Ndg. Mayaya Abraham Magese, Halmashauri ya Mji wa Bunda pamoja na Taasisi zinazofanya kazi ndani ya Halmashauri zimepongezwa kwa Utekelezaji na Usimamizi mzuri wa fedha za Miradi ya Wananchi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa.
Aidha Kamati imeelekeza Watendaji wa Kata kushiriki katika Baraza la Madiwani ili kuwajengea uwezo wa nini kinachohitajika wakiwa kama sehemu ya wanaoandaa taarifa hizo lakini pia kusikia na kupokea maazimio yanayotolewa.
Mbali na pongezi hizo, Kamati ya Siasa imetoa ushauri na maelekezo kwa baadhi ya Miradi iliyokaguliwa kama inavyoonekana hapo chini;
Choo Cha wanafunzi S/M Chiringe maji yafikishwe pamoja na umeme, lakini pia Halmashauri ikakague jengo linalohitaji marekebisho katika shule hiyo.
Barabara ya BDDH Nyamakokoto mradi ukamilike haraka, vitafutwe vyanzo vingine vya mapato ili fedha itumike kujenga mitaro kwaajili ya kuimarisha Barabara.
Mradi wa Maji Manyamanyama Mugaja Wananchi na Taasisi zinazonguka mradi wasambaziwe maji kwa haraka.
Ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Bitaraguru Halmashauri itafute fedha za umaliziaji wa jengo hilo.
Zahanati ya Mine ikamilishwe mapema, Changamoto ya Barabara na Umeme itatuliwe mapema katika eneo hilo.
Ukamilishaji wa Darasa shule ya Msingi Mcharo, Kamati imepongeza kwa usimamizi mzuri wa fedha za Mradi.
Msitu unaozunguka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wajumbe wameridhia kutunzwa ili uwe msitu tengefu
Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi zipatikane fedha za ukamilishaji wa Maeneo yote yaliyobaki.
Mradi wa Maji Kinyambwiga Guta ukabidhiwe kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Bunda kumalizia kupitia fedha zilizoombwa na RUWASA.
Mradi wa Sekondari ya kata ya Bunda Mjini Mradi utunzwe, Matokeo yanafanane na uzuri wa shule, Mazingira yatunzwe kwa kupanda miti na maua ya kutosha.
Mwisho, Serikali kupitia Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dkt. Vicent Anney amepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
20.05.2024
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda