Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Bunda ikiongozwa na Mwenyekiti Ndg. Mayaya Abraham Magese imetembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na kupongeza Mamlaka zinazosimamia miradi hiyo.
Mbali na pongezi, Kamati ya Siasa imetoa maelekezo pale ambapo kulikua na changamoto ili Mamlaka iweze kushughulikia na kwa miradi ambayo inaweza kushirikisha nguvu za Wananchi basi Viongozi wa eneo husika wawashirikishe ili waweze kushiriki katika mradi wao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda pamoja na Viongozi wa Taasisi wameiahidi Kamati ya Siasa kutekeleza maelekezo yote waliyotoa na kukamilisha miradi kwa ubora na ufanisi mkubwa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda